Wananchi bado hawajamkatia tamaa Dube

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2025
Wananchi bado hawajamkatia tamaa Dube

Msimu uliopita haukuanza vyema sana kwa mshambuliaji Prince Bube alilazimika kusubiri kwa takribani mechi 5 kwenye ligi kufungua akaunti yake mabao.

Jinamizi hilo bado linamuandama Dube ambaye msimu huu katika mechi tatu za ligi hajafunga bao lolote ingawa katika mechi za awali ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete Sc alifunga moja ya mabao katika ushindi wa mabao 3-0 kule Angola.

Pamoja na changamoto hiyo, mashabiki wa Yanga bado wanaonyesha kuwa na imani na Dube na bado hawajachoka kumpambania.

Ilishuhudiwa baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, mashabiki walimtuza Dube kwa kumchangia fedha huku wakimpa moyo aendelee kupambana.

Hamasa hii inaweza kumrejesha Dube katika makali yake na pengine katika mechi zijazo mabao yataanza kumiminika.

Licha ya Yanga kumsajili Andy Boyeli, bado Dube ameendelea kuwa mshambuliaji kiongozi hasa katika kipindi ambacho Clement Mzize bado ni majeruhi.

Msimu huu haujaanza vyema sana kwa Mzize ambaye pia muda mwingi ameutumia akiuguza jeraha la goti.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’