Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves ana jukumu la kukiandaa kikosi chake tayari kwa mikiki mikiki ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu
Katika droo iliyofanyika Afrika Kusini mapema leo Yanga imepangwa kundi B sambamba na klabu za Al Ahly, FAR Rabat na JS Kabylie. Yaani ni Yanga dhidi ya timu kutoka Afrika ya Kaskazini, mkakati ukiwa kufuzu robo fainali

Pedro ana kazi ya kufanya katika muda wa wiki mbili zilizosalia ili kuhakikisha Yanga inakuwa tayari kwa mikiki mikiki hiyo
Kiuhalisia Yanga haikuanza vyema msimu huu na ililazimika kusubiri mechi ya mwisho kutinga makundi mbele ya Silver Strikers ya Malawi ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 baada ya kupoteza kwa bao 1-0 katika mechi ya mkonodo wa kwanza.
Msimu uliopita Yanga haikuanza vyema hatua ya makundi ikipoteza mechi mbili za kwanza ikishuhudiwa kukosa nafasi ya kutinga robo fainali
Kundi B ukiondoa Al Ahly, unaweza kusema Yanga, AS FAR na JS Kabylie zote zina nafasi sawa na kuwania tiketi ya kutinga robo fainali, hapa mkakati ni kutumia vyema dimba la Mkapa