Mlinzi wa kushoto wa Yanga Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' leo amebeba tuzo ya nyota wa mchezo baada ya kuiongoza Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Zimbwe Jr alifunga bao la kwanza huku akionyesha kiwango bora katika mchezo huo ambao ushindi wa Yanga ulitokana na mashuti ya mbali kutoka kwa Zimbwe Jr na Ecua Celestin
Hii ni tuzo ya kwanza kwa Zimbwe Jr ambaye alijiunga na Yanga katika dirisha lililopita akitokea klabu ya Simba
Ama kwa hakika huu ni mwanzo mzuri kwake akiendelea kuwafunga midomo wakosoaji wake



ADVERTISE HERE