Pedro ajipanga kurejesha heshima na utambulisho wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2025
Pedro ajipanga kurejesha heshima na utambulisho wa Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves tayari ameanza majukumu yake akikiandaa kikosi kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumanne, Oktoa 28 katika uwanja wa KMC Complex.

Kama taratibu zake za vibali zitakuwa zimekamilika, Goncalves huenda akasimama kwenye benchi kwa mara ya kwanza katika mchezo huo ambao Yanga inahitaji kushinda baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana katika mchezo uliopita.

Lakini kama kuna mambo yatakuwa hayajakamilika, kocha Patrick Mabedi anaweza akaendelea kuonekana katika benchi la ufundi.

Mabedi anaendelea kuhudumu kama mmoja wa makocha wasadizi katika benchi la ufundi ambalo linaongozwa na Pedro aliyetua na kocha mwingine msaidizi Philipe Pedro na kocha wa makipa Fernando Pereira.

Jukumu la kwanza la Goncalves ni kuhakikisha anarejesha utamaduni wa Yanga kushambulia kwa kasi na kutawala mchezo. Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa Goncalves nae hupendelea kucheza soka la aina hiyo

Yanga chini ya Pedro inaweza kutumia mifumo mitatu tofauti ambayo kocha huyo ameitumia katika majukumu yake ya timu ya Taifa ya Angola yaani 4-4-2, 3-5-2 au 4-2-3-1.

Falsafa ya kocha huyo ni kuona timu yake inacheza soka la nidhamu la kuvutia, ikiwa na mipango sahihi ya kuzuia na kushambulia.

Mfumo wa 4-2-3-1 hautakuwa mpya kwa wachezaji wa Yanga kwani makocha waliopita Nasreddine Nabi, Miguel Gamondi, Sead Ramovic na hata Hamdi Miloud waliutumia.

Goncalves hatakuwa na muda kwani anakabiliwa na mechi tatu za ligi katika kipindi cha wiki moja dhidi ya Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na KMC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’