Wananchi hii ni mechi yetu ya kutupeleka makundi - Job

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2025
Wananchi hii ni mechi yetu ya kutupeleka makundi - Job

Nyota wa Yanga wameendelea kuwahamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo dhidi ya Silver Strikers kuwania kufuzu hatua na makundi ligi ya mabingwa (CAFCL)

Yanga imejichimbia Avic Town ikiendelea na maandalizi yake zikisalia siku mbili kuelekea mchezo huo

Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema wachezaji wako tayari na wangependa kuona uwanja wa Benjamin Mkapa unapambwa na rangi za Wananchi siku ya Jumamosi

"Tunatoa shukrani za dhati kwa viongozi wetu kwa kukubali mapendekezo ya mashabiki wetu kwa kutoa mchezo huu bila kuwa na kiingilio'

"Ningependa kuwaomba Wananchi, mapendekezo yenu yamekubaliwa na uongozi nasi tunarudi kwenu kuwaomba twende tukaujaze uwanja kwenye mchezo huo wa Jumamosi kwa sababu ni mchezo mkubwa na muhimu sana kwetu"

"Sisi kama wachezaji tunajiandaa vyema ili kuhakikisha tunapata ushindi. Wananchi huu ni mchezo wetu wa kutupeleka hatua ya makundi," alisema Job

Yanga inawahitaji mashabiki 60,000 siku ya Jumamosi kuwaongezea wachezaji hamasa ili kupata matokeo muhimu ya kuwavusha Wananchi hatua ya makundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’