Mabedi apewa mtihani dhidi ya Silver Strikers

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Oct 2025
Mabedi apewa mtihani dhidi ya Silver Strikers

Yanga inaingia kambini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya Silver Strikers utakaopigwa Jumamosi Oktoba 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Msaidizi Patrick Mabedi anakaimu nafasi ya Kocha Mkuu wakati uongozi ukiendelea na mchakato wa kumsaka mrithi wa Romain Folz aliyeonyeshwa mlango wa kutokea baada ya kipigo cha ugenini dhidi ya Silver Strikers.

Inaelezwa uongozi wa Yanga umemkabidhi Mabedi jukumu la kuiandaa timu na kuivusha hatua ya makundi huu ukiwa mtihani wake wa kwanza tangu alipojiunga na mabingwa hao wa nchi wiki iliyopita.

Mabedi anashirikiana na makocha wengine waliobaki katika benchi la ufundi baada ya Folz na Manu Rodriguez kuondoka.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Malawi kama atabadili upepo na kurejesha ile Gusa Achia Twenda kwao ya Wananchi na kuipeleka Yanga hatua ya makundi (CAFCL) anaweza kukabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga moja kwa moja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’