Kulikuwa na hofu juu ya mshambuliaji Clement Mzize kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Bingu huko Malawi
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa kuna uwezekano mkubwa Mzize akawa tayari kuikabili Silvers Strikers hapo kesho baada ya kuimarika
Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema Mzize anaimarika kwa haraka kuliko walivyotarajia na pengine huenda akawa tayari kushuka dimbani hapo kesho
"Mzize ametoka kwenye majeraha, alianza mazoezi siku chache zilizopita lakini tunafurahi kuona ameimarika kwa haraka"
"Leo (jana) ameweza kushiriki mazoezi ya timu, bado tuna siku moja zaidi ya mazoezi kabla ya mchezo, yapo matumaini anaweza kuwa tayari," alisema
Licha ya kuonekana akifanya mazoezi akiwa na bandeji kwenye mguu wake wa kushoto, Mzize alishiriki program za mazoezi ya kwanza Malawi