Nyota watatu wa Yanga Pacome Zouzoua, Prince Dube na Duke Abuya walitua nchini Malawi jana usiku tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers utakaopigwa kesho Jumamosi dimba la Bingu
Wachezaji hao walichelewa kurejea kutoka kwenye majukumu ya timu za Taifa
Kikosi cha Yanga kilitua Malawi mapema jana ambapo jioni walifanya mazoezi yao ya kwanza kujiandaa na mchezo huo
Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema wachezaji hao wameandaliwa program maalum ya 'recovery' ili kuhakikisha wanakuwa tayari kutumika siku ya kesho
Yanga itakamilisha maandalizi yake ya mwisho leo katika dimba la Bingu ambapo mchezo dhidi ya Silver Strikers utapigwa hapo kesho
ADVERTISE HERE