Manu aliomba kuondoka Yanga baada ya changamoto ya kiafya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Oct 2025
Manu aliomba kuondoka Yanga baada ya changamoto ya kiafya

Jana klabu ya Yanga ilimtangaza Patrick Mabedi kuwa kocha msaidizi akiungana na Romain Folz katika benchi la ufundi la mabingwa hao wa soka Tanzania Bara. Ikumbukwe Yanga tayari ilikuwa na kocha msaidizi Manu Rodriguez raia wa Hispania.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe amesema ujio wa Mabedi umefanikishwa baada ya ombi la Manu ambaye aliomba kuondoka baada ya kupata changamoto za kiafya

Kamwe amesema baada ya majadiliano baina yake na uongozi, ombi lake limekubaliwa na ndipo mchakato wa kumpata mbadala wake ukaanza

"Ni kweli Manu aliomba apewe ruhusa arejee kwao (Hispania) kushughulikia changamoto za kiafya. Baada ya ombi lake kuridhiwa uongozi ulianza mchakato wa kumpata mbadala wake ambaye ni rasmi sasa ametangazwa kocha Patrick Mabedi"

"Katika kipindi cha siku mbili hizi, Manu atarejea nchini kukamilisha taratibu za kiofisi na hapo tutakuwa tumeachana nae rasmi," alisema Kamwe

Baada ya kutambulishwa jana, Mabedi alianza majukumu yake akiungana na kocha mkuu Romain Folz ambaye sasa atapata msaada mkubwa kutoka kwa kocha huyo raia wa Zimbabwe

Mabedi ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika, amecheza na baadae kufundisha kazi yake ya mwisho kabla ya kujiunga na Yanga akiwa kocha wa timu ya Taifa ya Malawi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’