Hersi azidi kuchanja mbuga Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2025
Hersi azidi kuchanja mbuga Kimataifa

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye pia Mwenyekiti wa umoja wa klabu barani Afrika (ACA) yuko jiji la Rome Italia akihudhuria mkutano wa umoja wa klabu barani Ulaya (ECA)

Hersi amesema amepewa heshima ya kipekee kushuhudia historia katika ushirikiano wa klabu barani Ulaya ikiandikwa

"Katikati ya jiji la Roma, Italia, nilipata heshima kubwa ya kushuhudia historia ikiandikwa wakati European Club Association (ECA) ikibadilishwa rasmi kuwa European Football Club (EFC)."

"Mkutano huu wa kihistoria uliwakutanisha watu wenye akili na ushawishi mkubwa katika soka, akiwemo Rais wa FIFA Gianni Infantino na Mwenyekiti wa EFC Nasser Al-Khelaifi."

"Huu ni mwanzo wa enzi mpya kwa soka la Ulaya, na kama Mwenyekiti wa African Club Association (ACA), nina furaha kubwa kujenga madaraja ya ushirikiano na kujifunza kutoka katika safari ya EFC."

"Pamoja, tutaibadilisha ACA na kuinua hadhi ya soka la vilabu barani Afrika kufikia viwango vya juu zaidi," aliandika Hersi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’