Kikosi cha Yanga Princess jioni ya leo kitashuka dimba la KMC Complex kuikabili JKT Queens katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii
Hakuna unyonge msimu huu ndio kauli ya Wananchi kuelekea mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni
Habari njema kwa Yanga Princess ni kuwa mshambuliaji Jeanine Mukandayisenga atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili JKT Queens leo. Ni baada ya jaribio la kutaka mshambuliaji huyo azuiwe kugonga mwamba
Jana Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) lilitoa ufafanuzi wa vipimo ambavyo vitafanyika kubaini uhalisia wa jinsia kwa wachezaji wanaolalamikiwa
Hata hivyo TFF imebainisha kuwa utaratibu huo utaanza kutumika kuanzia msimu ujao (2026/27), hivyo msimu huu hakuna mchezaji atazuiwa
Ikumbukwe Yanga pia iliwasilisha malalamiko TFF ikiomba wachezaji 15 wa Simba Queens wafanyiwe vipimo baada ya kuwatilia mashaka