Baada ya mapumziko ya siku chache kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kuanza maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya Silver Strikers ya Malawi
Oktoba 18 Yanga itakuwa ugenini huko Malawi kucheza mechi ya mkondo wa kwanza na mechi ya marudiano kufanyika jijini Dar es salaam wiki moja baadae
Mazoezi ya Yanga leo yanatarajiwa kusimamiwa na kocha mkuu Romain Folz ambaye licha ya tetesi nyingi zinazohusu hatma yake, bado yuko na Wananchi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mpaka sasa hakuna mabadiliko yaliyofanyika kwenye benchi la ufundi kwa hiyo Folz ataendelea na majukumu yake
Yanga inarejea mazoezini leo bila ya nyota wake 12 ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota hao ni Djigui Diara aliyeitwa Mali, Israel Mwenda, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Aziz Andabwile na Offen Chikola walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Wengine ni Duke Abuya (Kenya), Lassine Kouma na Celestin Ecua (Chad), Prince Dube (Zimbabwe) na Pacome Zouzoua (Ivory Coast)
Wachezaji hao watarejea kikosini baada ya kuhitimishwa kalenda ya FIFA ambapo mechi za mwisho zitapigwa Oktoba 14