Nafasi adimu kwa Folz kujipanga upya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2025
Nafasi adimu kwa Folz kujipanga upya

Baada ya mapumziko ya siku chache, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini siku ya Jumatatu kuanza maandalizi ya mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers.

Unaweza kusema wakati huu wa mapumziko ya kalenda ya FIFA, ni wakati mzuri sana kwa Yanga kujipanga.

Baada ya matokeo ya mchanganyiko kwenye michezo ya mwanzo wa msimu, mapumziko ya FIFA yanampa kocha Romain Folz nafasi ya dhahabu ya kujipanga upya, kurekebisha mikakati na kumaliza changamoto ambazo zimekuwa zikiwakera mashabiki hadi sasa.

Mashabiki wameonyesha hofu yao, kama uongozi wa Yanga utampa Folz nafasi ya kurekebisha, ni wazi anafahamu nini anapaswa kufanya.

Wanayanga wanaifahamu vyema timu yao katika misimu hii minne, inashinda na kucheza soka la kuvutia. Hata pale inapopoteza na hata kutoka sare, mashabiki wanafahamu kama ni matokeo ya mpira wa miguu au la.

Mapumziko haya pia ni nafasi ya wachezaji kujipanga upya na kusahihisha yale yote ambayo hawakufanya vyema. Mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ni Oktoba 18. Hakuna timu ndogo baada ya hatua ya awali, malengo ya Yanga ni kutinga hatua ya makundi.

Ni wazi Folz yupo chini ya shinikizo, lakini sasa amepata angalau wiki mbili kuandaa kikosi chake kwa mapambano yaliyo mbele. Iwapo atatumia vyema mapumziko haya, anaweza kuirejesha Yanga ikiwa imara zaidi na kuwanyamazisha wakosoaji wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
24m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’