Majeraha kumweka nje Mzize wiki tatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2025
Majeraha kumweka nje Mzize wiki tatu

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, atakaa nje ya dimba kwa muda wa kati ya wiki tatu hadi nne kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata hivi karibuni.

Mzize, ambaye msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara alipachika mabao 14, alipata jeraha hilo wakati Yanga ikiichapa Wiliete SC ya Angola mabao 3-0 kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Daktari wa timu ya Yanga, Moses Etutu, amesema kuna matumaini makubwa ya Mzize kurejea dimbani baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Kuumia kwa Mzize pia kumeathiri kikosi cha Taifa Stars, ambacho kinajiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zambia utakaopigwa Oktoba 8 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ amelazimika kumwacha nje ya kikosi kutokana na jeraha hilo.

Msimu huu Mzize ameitumikia Yanga katika mechi mbili Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete SC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’