Mchezo wa ligi kuu kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Sokoine Mbeya umemalizika kwa maatokeo ya suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa mchezo uliochezwa kwa kasi ya chini pengine hali ya dimba la Sokoine limechangia kwa hali hiyo
Kidogo Yanga iliongeza kasi kwenye kipindi cha pili lakini Mbeya City walikuwa imara zaidi katika kujilinda huku wakitumia mashambulizi ya kushitukiza
Ni alama moja muhimu ambayo pia unaweza kumpongeza mlinda lango Djigui Diarra ambaye aliokoa shambulizi la hatari dakika za lala salama kuinusuru Yanga na kipigo






ADVERTISE HERE