Andabwile afichua siri ya ubora wake msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2025
Andabwile afichua siri ya ubora wake msimu huu

Kiungo wa Yanga, Aziz Andabwile, ameibuka kama moja ya nyota wanaokipa moto kikosi cha kocha Romain Folz msimu huu, akifichua siri ya mafanikio yake ni kujitoa, kushirikiana na wenzake pamoja na kufuata maelekezo ya mwalimu.

Andabwile amesema falsafa yake ni rahisi, anatimiza majukumu yake kwa kuzingatia maelekezo ya mwlimu na pia anashirikiana na wachezaji wenzake

“Kikubwa ni kutimiza majukumu yangu, lakini sifanyi peke yangu. Ushirikiano na wenzangu na kufuata maelekezo ya kocha ni msingi wa mafanikio ya Yanga. Kiu ya kila mmoja ni kutoa mchango wake,” alisema

Katika michezo minne ya mashindano ambayo Yanga imecheza msimu huu, Andabwile ameshuka dimbani mara tatu akicheza dakika zote 90, huku mara moja akitokea benchi dhidi ya Pamba Jiji.

Amefunga mabao mawili muhimu dhidi ya Wiliete ya Angola, akitikisa nyavu ugenini na kuhitimisha nyumbani jambo lililowafanya mashabiki wamwone kama shujaa mpya Jangwani.

Yanga ilianza kampeni zake kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba, ikashinda 3-0 dhidi ya Wiliete ugenini, na kisha kufunga safari ya marudiano jijini Dar es Salaam kwa ushindi wa 2-0. Katika michezo hiyo, Andabwile aliendeleza kiwango cha juu.

Msimu uliopita haukuwa mzuri kwake. Andabwile alipata nafasi finyu chini ya makocha watatu waliopita (Miguel Gamondi, Sead Ramovic na Miloud Hamdi), akicheza mechi tano pekee na dakika 125 bila kufunga wala kusaidia bao.

Lakini chini ya Folz, amebadilika na kujipanga upya, akiashiria kuwa huu unaweza kuwa msimu wake wa kuthibitisha uwezo mkubwa alionao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’