Wakati Nasreddine Nabi anainoa Yanga alipendwa na Wananchi kutokana na kazi yake nzuri uwanjani na sifa ya kuamini na kuwaendeleza wachezaji wa ndani
Wachezaji kama Ibrahim Bacca, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Mudathir Yahya, Kibwana Shomari, Clement Mzize, Salum Abubakar, Farid Mussa na wengine walipata nafasi na kuaminiwa na Nabi
Unaweza kusema kocha Romain Folz ni kama anarejesha utamaduni huo kwani nae anatoa nafasi na kuwaamini wachezaji wa ndani
Katika mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete Sc, wachezaji nane wa ndani walipata nafasi ya kucheza
Katika kikosi kilichoanza aliwajumuisha Kibwana Shomari, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Aziz Andabwile na Mudathir Yahya huku Shekhan Khamis, Offen Chikola na Edmund John wakiingia katika kipindi cha pili
Ubora anaoonyesha Andabwile sasa unaweza kusema ni kazi nzuri ya Folz ambaye alimuamini tangu siku ya kwanza, pengine sasa hakuna shabiki wa Yanga ambaye anaweza kuhoji kiungo huyo anapoonekana kikosini
Andabwile ndiye kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa akiwa amefunga mabao mawili na ni kiungo mkabaji!
Kama sio Folz pengine Andabwile asingekuwa Yanga kwani hata mashabiki walikuwa wamemkatia tamaa wakiamini hana uwezo wa kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara