Pacome Zouzoua alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba jana pengine kwa kuwa alifunga bao pekee lililoihakikishia Yanga ushindi wa bao 1-0
Lakini kama isingekuwa hivyo mlinda lango Djigui Diarra, alipaswa kushinda tuzo hiyo baada ya kazi nzuri aliyofanya uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kuiweka Yanga mchezoni na hatimaye kuibuka na ushindi baada ya dakika 90
Ziko nyakati Yanga ilihitaji uimara wake langoni, akiokoa nafasi takribani tatu za wazi ambazo pengine angekuwa mlinda lango legelege ingekuwa siku mbaya sana
Huyu hakuitwa 'Screen Protector' au 'Mdaka Mishale' kwa bahati mbaya, majina hayo yanaakisi kile anachokifanya langoni




ADVERTISE HERE