Ecua mapema tu Wiki ya Mwananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Sep 2025
Ecua mapema tu Wiki ya Mwananchi

Kuonyesha kuwa amepania kuwapa burudani mashabiki wa Yanga kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi Ijumaa Septemba 12, kiungo mshambuliaji Celestin Ecua aliondoka kambi ya timu ya Taifa ya Chad baada ya mchezo dhidi Ghana

Juzi Chad walicheza dhidi ya Madagascar wakikubali kipigo cha mabao 3-1 lakini Ecua hakuwa sehemu ya mchezo huo baada ya kuondoka kambini mapema

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zimebainisha kuwa Ecua aliwapigia simu mabosi wa timu hiyo akiwaambia anataka kuwahi Dar kutoka kambi ya timu ya taifa ili apate maandalizi kabambe kuelekea Tamasha la Wiki ya Mwananchi na mchezo wa Ngao ya Jamii.

Ecua aliwaambia mabosi wa Yanga, kama Chad itachelewa kumtumia tiketi ya ndege basi, klabu yake ikae tayari kumtafutia haraka kwani anataka kuwahi nchini.

“Ecua amepiga simu anasema amemwomba meneja wa timu ya taifa lake ahakikishe anaondoka Madagascar mara baada ya mchezo kumalizika, wakamwambia sawa,” kilisema chanzo hicho.

“Licha ya jibu hilo, Ecua akaona atupigie ili tujiandae kama Chad wakichelewa kumtengenezea tiketi hiyo, sisi huku tumfanyie wepesi kumpa tiketi ya kumtoa kule haraka ili awahi Tamasha la Wiki ya Mwananchi," kilieleza chanzo

Ecua aliitumikia Chad kwenye mchezo dhidi ya Ghana akifunga bao la kusawazisha katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza kuitumikia Chad tangu alipobadili uraia wake kutoka Ivory Coast

Wachezaji wote waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wanatarajiwa kuripoti kambini kuanzia leo siku mbili kabla siku ya Tamasha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
32m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
41m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’