Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepoteza matumaini ya kufuzu kombe la Dunia 2026 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Niger katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar
Unaweza kusema Stars leo ilicheza chini ya kiwango, licha ya kuhitaji ushindi katika mchezo huo, morali ya timu haikuonekana kwa muda mwingi wa mchezo
Pengine uchovu wa wachezaji umechangia vijana hao wa Suleiman Morocco kucheza chini ya kiwango leo hasa ikizingatiwa sehemu kubwa ya wachezaji walioitwa wametoka kushiriki michuano ya CHAN 2024
Tanzania ilihitaji kushinda leo ili kuweka hai matumaini ya kukata tiketi ya play-off baada ya Morocco kujihakikishia kufuzu moja kwa moja baada ya kuongoza kundi E
Niger ni kama wamelipa kisasi cha kipigo cha bao 1-0 walichokipata kutoka kwa Stars katika mchezo wa raundi ya kwanza
Nyota wa Yanga waliokuwa katika kikosi hicho sasa wanarejea Avic Town kuungana na wenzao kuelekea Yanga Day siku ya Ijumaa
