Thamani ya Yanga ni Bilioni 100

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2025
Thamani ya Yanga ni Bilioni 100

Klabu ya Yanga ina thamani ya Shilingi Bilioni 100, baada ya kamati maalum iliyoundwa kwa ajili ya tathmini hiyo kukamilisha kazi yake.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa SuperDome, Masaki jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alex Mgongolwa, alisema tathmini hiyo imefanywa na kampuni ya kimataifa ya ushauri wa uwekezaji na mali isiyohamishika, Colliers International.

Mgongolwa alisema hatua hiyo ni mwanzo wa mchakato mpana wa klabu kuingia katika mfumo wa kisasa wa uendeshaji kwa kuuza hisa, na kuongeza kuwa thamani hiyo itatumika kama mwongozo katika taratibu zote za uwekezaji zitakazoanza hivi karibuni.

Kwa mara ya kwanza, Yanga inakuwa miongoni mwa vilabu vichache nchini vilivyopata uthamini rasmi wa kibiashara, hatua inayotajwa kufungua ukurasa mpya wa uendeshaji wa kisasa

Thamani hiyo ni mara tano ya thamani ya watani zao klabu ya Simba iliyo na thamani ya Tsh Bilioni 20

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’