Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa klabu ya Yanga unafanyika leo Jumapili, Septemba 07 ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es salaam
Mkutano huo utarushwa mbashara na Azam Tv kuanzia saa 3 asubuhi
Mkutano mkuu huo umeitishwa kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya katiba ya klabu hiyo ya 2021, huku ukiwa na ajenda 10
Ajenda 10 za mkutano huo ambao awali ulitangazwa na Rais wa klabu hiyo, Hersi Said mapema Agosti 8, mwaka huu, ni pamoja na ile ya ufunguzi, uhakiki wa wajumbe, kuthibitisha ajenda na kumbukumbu za mkutano uliopita.
Nyingine ni yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita, hotuba ya Rais, kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji, kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangu-lia pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya klabu, kuthibitisha bajeti kwa mwaka unaofuata na kufunga mkutano