Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa mlinzi wa pembeni wa Yanga Kibwana Shomari
Tangu ajiunge na Wananchi akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, Kibwana sasa ameitumikia Yanga kwa takribani misimu minne
Kibwana ni mchezaji ambaye unaweza usimuone uwanjani mara kwa mara lakini siku utakapomuona una uhakika na kile anachokwenda kukifanya
Baada ya Yanga kumsajili Yao Kouassi, muda wake wa kucheza ulipungua sana lakini sasa ni kama amerejea tena katika nafasi yake akipishana na Israel Mwenda wakati Yao akiendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
HAPPY BIRTHDAY KIBWANA...!
ADVERTISE HERE