Klabu ya Yanga imetangaza uzinduzi wa kilele cha wiki ya Mwananchi utafanyika kesho Jumatano, viwanja wa Zakhiem Mbagala jijini Dar es salaam
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya Yanga mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo utakaoanza saa 5 asubuhi
Kamwe pia ametangaza viingilio vya kilele cha wiki ya Mwananchi itakayofanyika Septemba 12 pale uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga itachuana na Bandari Fc ya Kenya
"Viingilio VVIP - 600,000/-, Royal - 300,000/-, VIP A - 50,000/-, VIP B - 30,000/-, VIP C - 15,000/-, Machungwa - 10,000/- na Mzunguuko - 5,000/-"
"Ukataji tiketi umerahisishwa na pia hata utaratibu wa kuingia uwanjani nao umerahisishwa. Huduma mbalimbali zitapatikana kwa urahisi uwanjani na pia tumefanyia kazi mapendekezo ya maboresho upande wa burudani"
"Kutakuwa na mechi tatu zitakazohusisha timu ya Wanawake, timu ya viongozi dhidi ya Wasanii na mechi kati ya Yanga dhidi ya Bandari Fc"
'Uzinduzi rasmi wa hamasa kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi utafanyika kesho Jumatano katika viwanja vya Zakhiem Mbagala kuanzia saa 5 asubuhi ambapo pia kutakuwa na maeneo maalum ambayo tiketi zitakuwa zikiuzwa," alisema Kamwe
Kamwe ametangaza kauli mbiu ya Wiki ya Mwananchi 2025 ni TUNAPIGA KICHWANI TU, amesema kaulimbiu hiyo itatumika msimu mzima 2025/26