Kamwe ataja sababu kilele Wiki ya Mwananchi kuwa Ijumaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2025
Kamwe ataja sababu kilele Wiki ya Mwananchi kuwa Ijumaa

Ijumaa ya Septemba 12 2025 ndio kilele cha Wiki ya Mwananchi, tukio kubwa la burudani ukanda wa Afrika Mashariki na kati likifanywa na klabu ya Yanga

Hili ni tukio la kukaribisha msimu mpya ambapo maefu ya Wanayanga watakutana uwanja wa Benjamin Mkapa na wengine kulishuhudia katika runinga zao

Lakini mwaka huu tukio hilo linafanyika Ijumaa na sio siku za mwisho wa wiki yaani Jumamosi au Jumapili kama ilivyozoeleka

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amefichua kuwa hata kuipata tarehe 12 haikuwa rahisi kutokana na changamoto ya ratiba

“Tayari klabu imeshatangaza tarehe ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi ambayo ni tarehe 12/9/2025, wengi wenu mmekuwa mkijiuliza kwanini Tamasha hili linafanyika siku ya Ijumaa na siyo jumamosi au jumapili kama ilivyozoeleka?"

"Niwaambie tu ndugu zangu, hawa viongozi wetu wamepambana sana mpaka tamasha hili kuwepo msimu huu kwa sababu ratiba za mechi za kalenda ya FIFA zimebana sana"

"Kama tungepanga tarehe nyingine basi tungewakosa wachezaji wetu wengi ambao wameitwa kwenye timu zao za timu za Taifa. Mbali na hapo kuna ratiba ya Ngao ya Jamii na Ligi, hivyo tusingepanga tarehe 12 basi tungekuwa na wakati mgumu kuipata burudani hii ya kilele cha Wiki ya Mwananchi,” alisema Kamwe katika mkutano maalum na Wazee, viongozi wa matawi Dar na makundi ya mitandao ya kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’