Muhimu wasikimbie tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2025
Muhimu wasikimbie tu

Tarehe 16 Septemba, macho yote yatakuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo miamba ya soka nchini Yanga SC na Simba SC watakutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Mchezo huu maalum kila msimu huwa fursa ya kufungua pazia la msimu mpya huku mapato yake yakielekezwa kwenye kusaidia jamii.

Hata hivyo, kumeibuka hofu baada ya tetesi kuwa Simba wameomba mchezo huo usogezwe mbele kutokana na ratiba yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo wanatarajiwa kucheza Botswana dhidi ya Gaborone United mnamo Septemba 20. Lakini hoja kubwa inayoibuka ni je, huu ni ukweli wa ratiba pekee au ni hofu ya kukutana na Yanga mapema kabla ya msimu kuanza?

Mashabiki hawajasahau Machi 8 msimu uliopita, ambapo Simba walishindwa kujitokeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga. Mchezo huo ulisogezwa mara kadhaa kabla ya kupigwa Juni 25 katika Uwanja wa Mkapa, ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Huo ulikuwa ushindi wa tano mfululizo kwa Yanga dhidi ya Simba, rekodi inayozidi kuumiza mashabiki wa Msimbazi.

Sasa, iwapo Simba watakutana na Yanga Septemba 16 na kufungwa tena, itakuwa ni mara ya sita mfululizo kwa wekundu wa Msimbazi kupoteza dhidi ya watani wao. Hali hiyo inaweza kuleta mtafaruku mkubwa ndani ya klabu na miongoni mwa mashabiki wao.

Yanga wametumia dirisha la usajili kwa ufanisi mkubwa, wakiongeza nguvu mpya ikiwemo kumsajili beki kisiki na aliyekuwa nahodha wa Simba, Mohammed Hussein β€œZimbwe Jr”. Usajili huu pekee ni pigo la kisaikolojia kwa Simba kabla hata hawajakutana uwanjani.

Kwa upande mwingine, tetesi za Simba kutaka mchezo usogezwe mbele zinaacha maswali mengi. Je, ni kweli ni ratiba ya CAF Champions League inayowabana, au ni hofu ya kuingia uwanjani dhidi ya Yanga wakiwa hawajapata uthabiti wa kikosi?

Mchezo wa Ngao ya Jamii si tu pambano la jadi bali pia lina dhamira kubwa ya kijamii. Mapato yake yanasaidia sekta mbalimbali za jamii, jambo linaloongeza uzito wa klabu zote kushiriki bila visingizio.

Simba wanapaswa kuthibitisha kuwa wao bado ni wakubwa wa soka la Tanzania kwa kuingia uwanjani na kupambana na Yanga, bila hofu wala visingizio. Mashabiki wanahitaji kuona vita ya jadi ikiendelea, si kuona timu kubwa ikijitahidi kuepuka kukutana na mpinzani wake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’