Wiliete Benguela sio wanyonge

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2025
Wiliete Benguela sio wanyonge

Wiliete Benguela ya Angola itachuana na Yanga katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika

Timu hiyo iliyoanzishwa miaka 8 iiliyopita, ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Angola nyuma ya Petro Atletico iliyotwaa ubingwa

Hii itakuwa mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya CAF, ni timu iliyoimara kiuchumi ikisajili wachezaji wenye wenye uzoefu na michuano hiyo mikubwa

Klabu hiyo ambayo pia imewasajili nyota waliowahi kutamba na Yanga Skudu Makudubela na Joyce Lomalisa, pia inatajwa kumuajiri kocha wa zamani wa Azam Fc, Bruno Ferry

Itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Septemba 21 huko Angola na marudiano kupigwa wiki moja baadae katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Wiliete Benguela imeweka kambi nchini Ureno ikijiandaa na mtanange huo ambao utaamua timu ya kusonga mbele raundi ya kwanza

Kwa kutambua ugumu wa mchezo huo, Yanga imeendelea na maandalizi yake Avic Town kujiweka sawa kuwakabili Waangola hao

Malengo ya Yanga ni kutinga hatua ya makundi ambapo wakifanikiwa wataweka mkakati mpya kwa hatua zinazofuata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
57m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’