Assink ni beki kiraka

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2025
Assink ni beki kiraka

Beki mpya wa Yanga Frank Assink tayari ameanza 'kukiwasha' pale Avic Town ambako kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi yake ya msimu mpya

Yanga imemsajili Assink akitokea klabu ya Singida Black Stars akichukua nafasi ya Yao Kouassi ambaye amepewa muda zaidi wa kujiimarisha baada ya upasuaji wa goti aliofanyiwa

Assink ni beki kiraka ambaye Yanga inaweza kumtumia katika nafasi yoyote kwenye safu ya ulinzi kwani licha ya kumudu vyema kucheza eneo la beki wa kati, pia anaweza kutumika kama mlinzi wa pembeni

Lakini pia usajili wake utawapa ahueni mabeki Dickson Job na Ibrahim Bacca ambao wametumika zaidi tangu msimu uliopita

Bacca na Job ni tegemeo sio kwa Yanga tu bali hata timu ya Taifa. Tangu msimu ulipomalizika, wachezaji hao hawajapata muda wa kupumzika

Ni juzi tu wametoka kushiriki michuano ya CHAN na kikosi cha Stars wakicheza mechi zote tano lakini wanakabiliwa na kazi nyingine katika timu ya Taifa mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Niger Septemba 09

Assink na nahodha Bakari Ndondo Mwamnyeto kwa wakati huu ndio tegemeo pengine wanaweza kutumika katika mechi za mwanzo wa msimu wakati Bacca na Job wakifanyiwa 'rotation' ili kulinda afya zao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’