Klabu ya Yanga iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa beki wa kati raia wa Ghana Frank Assinki kutoka Singida Black Stars, imefahamika
Assinki anajiunga Yanga kwa mkopo ambapo atawatumikia Wananchi msimu wote wa 2025/26
Yanga imefanya usajili huo kwa dharura baada ya kujiridhisha Yao Kouassi 'Jeshi' atahitaji muda zaidi kuimarika baada ya upasuaji wa goti aliofanyiwa
Yao ataendelea kusalia katika kikosi cha Yanga lakini hatajumuishwa katika usajili hadi wakati wa dirisha dogo Januari 2026, hivyo kwa sasa nafasi yake inachukuliwa na assinki ambaye anamudu vyema kucheza beki wa kati, beki wa kulia pamoja na kiungo mkabaji
Assinki alifanya vyema katika kikosi cha Singida BS msimu uliopita akiwa tegemeo katika safu ya ulinzi
Wananchi wamepita nae shwaaaaa...!