Jezi za 2025/26 ni mtoko kamili - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Aug 2025
Jezi za 2025/26 ni mtoko kamili - Kamwe

Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewaambia Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo wajiandae kupokea jezi bora za msimu ujao 2025/26

Kamwe amesema jezi za 2025/26 zimepandishwa kiwango cha ubora, ni vazi rasmi 'mtoko' ambao Mwananchi anaweza kuvaa hata kwenye matukio makubwa na muhimu

"Jezi mpya za Yanga ni 'mtoko', ni jezi ambazo tumepandisha viwango vya ubora na unaweza kuvaa sehemu yoyote"

"Tumezindua pre-order ambayo hii ni maalum kwa ajili ya wale ambao hawapendi usumbufu, hii inawahusu zaidi wafanyabiashara wa jumla wenye maduka makubwa na matawi ya Yanga"

"Wenyeviti wa matawi nchi nzima wanapaswa kutumia fursa hii kuweka oda ya jezi kwa ajili ya wanachama katika matawi yao"

"Oda ni angalau pisi 300 hivyo Viongozi wa matawi waratibu utaratibu wa wanachama wao wanaotaka jezi kujiandikisha na kulipia Tsh 32,000/-," alisema Kamwe

Yanga inatarajiwa kuzindua jezi mpya siku chache kabla ya Tamasha la wiki ya Mwananchi ambalo bado tarehe yake haijatangazwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’