Dakika 45 alizocheza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports, zimeonyesha ni kiasi gani mshambuliaji Andy Boyeli anaweza kuinufaisha Yanga msimu ujao
Boyeli alifunga bao la kusawazisha la Yanga katika mchezo huo ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 3-1
Lakini pia alitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Pacome Zouzoua ikiwa ni kama Boyeli alilipa fadhila aliyofanyiwa na Pacome alimyemtengenezea bao alilofunga
Kwa aina ya uchezaji wake, haitashangaza kumshuhudia Boyeli akifunga mabao mengi msimu ujao

Boyeli ni mshambuliaji asiye na mambo mengi, hucheza katika maeneo ya hatari na hahitaji nafasi nyingi kufunga
Mapema tu Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz ameonekana kufurahishwa na aina yake ya uchezaji akimuanzisha katika mchezo dhidi ya Rayon na baadae nafasi yake kuchukuliwa na Prince Dube kwenye kipindi cha pili
Boyeli na Dube wanatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga msimu ujao, huku Clement Mzize akisubiri hatma ya uhamisho wake kuelekea Esperance