Huyu Casemiro anaweza kuanza kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2025
Huyu Casemiro anaweza kuanza kikosi cha kwanza

Kiungo kinda Abdulnassir Mohammed 'Casemiro' ni miongoni mwa sajili zilizofanywa na Yanga katika dirisha hili

Casemiro ambaye aliibuka mchezaji bora chipukizi katika ligi kuu ya Zanzibar msimu uliopita, alitua Yanga akitokea klabu ya Mlandege

Wakati kiungo huyo mkabaji anasajiliwa sambamba na beki Abubakar Nizar Othman 'Ninju', wachezaji hao walitizamwa kama vijana wachanga ambao watahitaji muda kuendelezwa kabla ya kuanza kutumika ipasavyo katika kikosi cha kwanza

Lakini kutokana na kiwango wanachoonyesha kwenye mazoezi yanayoendelea pale uwanja wa KMC Complex, Kocha Mkuu wa Yanga Ramain Folz na benchi lake la ufundi wameshawishika kuwajumuisha katika kikosi cha kwanza na watachuana na wachezaji wengine kuwania nafasi kikosini

Casemiro amekuwa kivutio zaidi hata kwa wachezaji wenzake ambao baadhi wamekiri kuwa nyota huyo ana kipaji kikubwa na pengine atawashangaza wengi pale msimu utakapoanza

"Huyu kijana anajua sana mpira, anajituma na pia anapambana sana, ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kukimbilia pasi ya pili, akiendelea na nidhamu hii, hiki ni kipaji kikubwa sana," kiungo Maxi Nzengeli aliiambia Yanga TV

Mlinda lango Djigui Diarra nae alionekana kuvutiwa na kinda huyo mara kwa mara akionekana kumuelekeza baadhi ya mambo ya kiufundi ili azidi kuboresha kile anachofanya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’