Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameishukuru kampuni ya Haier kwa kuendeleza ushirikiano wake na klabu ya Yanga ambao umekuwa chachu ya mafanikio kwa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara
Akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba mpya wa udhamini leo, Hersi alisema Haier imekuwa sehemu ya mafanikio ya Yanga tangu walipoingia makubaliano ya udhamini miaka miwili iliyopita katika michuano ya kombe la Shirikisho ambapo Yanga ilifika hatua ya fainali
Hersi amesema mkataba huo mpya wa miaka mitatu, unaimarisha Yanga kiuchumi na utaongeza chachu zaidi kwa Yanga kuendelea kufanya vyema
"Leo ni moja ya siku ya kihistoria kwa Klabu yetu. Leo tunatangaza kuongeza mahusiano na Haier Tanzania, hii ni taarifa njema sana kwa Klabu yetu kwenye uimara wa kiuchumi wa timu yetu. Mkataba wa awali ulikuwa mzuri sana. Tulifanya vyema sana kwenye mashindano ya shirikisho ambapo tulifika fainali"
βUhusiano wa Haier na Yanga ulikuwa na Baraka kubwa. Ni matumaini yetu kuwa mkataba huu mpya utakuja na mafanikio zaidi. Msimu wa kwanza na Haier tulifika fainali ya Shirikisho Afrika. Mkataba huu utakuwa wa miaka mitatu mpaka mwaka 2028"
"Nembo za Haier zitakaa mkono wa kushoto kwenye mashindano ya ligi. Mkataba huu utakuwa na thamani ya Tsh bilion 3.3," alisema Hersi