Klabu ya Yanga imeridhia kumruhusu mshambuliaji wake Clement Mzize ajiunge na Al-Sadd SC ya Qatar, imefahamika
Al-Sadd SC wamewasilisha ofa rasmi kwa Yanga kwa ajili ya Mzize inayokadiriwa kufika Tsh Bilioni 2.2
Yanga imeiruhusu Al-Sadd SC kumalizana na Mzize upande wa maslahi binafsi kabla ya kukamilisha mchakato wa usajili
Kuna uwezekano mkubwa Mzize ataelekea Qatar kujiunga na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa michuano ya CHAN iliyoanza juzi Jumamosi
Aidha, Kwa usajili ambayo Yanga imefanya katika dirisha hili, ni kama ilikuwa imejipanga endapo Mzize ataondoka
Katika safu ya ushambuliaji Yanga imewaongeza Andy Boyeli na Ecua Celestin ambaye anaweza kutumika kama mshambuliaji wa kati au winga, nafasi ambayo Mzize amekuwa akitumika ndani ya Yanga