Boyeli achagua jezi namba 9, aahidi mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2025
Boyeli achagua jezi namba 9, aahidi mabao

Mshambuliaji wa Yanga Andy Boyeli amesema malengo ya klabu ndio sababu kuu iliyopelekea achague kujiunga na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara akitokea klabu ya Shekhukhune ya Afrika Kusini

Boyeli ambaye jina lake la utani ni 'tembo', ameeleza kuvutiwa na mipango ya Yanga na kikubwa zaidi ni timu kubwa Tanzania ikiwa na rekodi ya aina yake

"Kitu muhimu kwangu kilichopelekea kuwa hapa ni malengo ya klabu, lakini pia ukweli ni kwamba ni timu nzuri na inashinda makombe kila msimu. Matamanio ya kila mchezaji ni kushinda makombe"

"Pia niliongea na Rais wa Yanga (Injinia Hersi) nikajisikia amani kuja hapa Tanzania, kwani alinipa ujasiri kuja kufanya hazi hapa," alisema Boyeli

Boyeli amesema baada ya kutua Yanga, lengo lake ni kufunga mabao mengi na kuisaidia tiimu kufikia malengo yake

Mshambuliaji huyo amechagua kuvaa jezi namba 9 ambayo iliwahi kutumiwa na Mcongomani mwenzake Fiston Mayele

"Nitapambana na kuhakikisha nafunga mabao mengi nikiwa hapa, nimechagua kuvaa jezi namba 9. Natambua jezi hii iliwahi kuvaliwa na Fiston Mayele"

"Nimewahi kucheza ligi moja na Mayele kule Congo, yeye alikuwa akicheza AS Vita na mimi RC Rangers. Nimekuwa na mawasiliano naye hata alivyokuwa hapa Yanga"

"Mayele aliniambia Yanga ni timu kubwa zaidi hapa Tanzania na ina mashabiki bora, akanihakikishia nikiwa hapa nitafurahia," alisema Boyeli

Bayeli amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuisapoti timu na wachezaji wote huku akiwaahidi atapambana na kufanya majukumu yake vyema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’