Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amekanusha tetesi zinazosambaa mitandaoni kuhusu mshambuliaji Prince Dube akisisitiza mshambuliaji huyo hajaomba kuondoka Yanga
Kamwe amekanunusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa mapema Jumatano zikidai Dube anataka kuvunja mkataba wake kutokana na madai ya fedha za usajili
"Watu wanatafuta namna ya kutuzungumzia vibaya, ni taarifa za uzushi kwa asilimia 100. Watuambie Dube amekwenda kushitaki mamlaka zipi za mpira ndani au nje?"
"Prince Dube ni mchezaji wa Yanga mwenye mkataba wa mwaka mmoja, hizo mnazosikia ni stori ambazo watu wanatengeneza kututia ubaya baada ya kuona mambo yetu yamenyooka"
"Mimi kama msemaji wa taasisi na sauti ya Yanga siwezi kuwadanganya Wananchi wakati najua endapo Dube ataondoka itakuwa aibu kwangu"
"Taarifa hizo ni uzushi kama uzushi mwingine, masuala ya malipo ya mchezaji yanafanyika kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba" alisema Kamwe
Dube alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea klabu ya Azam Fc, ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili. Mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu ujao