Yanga imekamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City Rafael Daudi 'Alpha', amesaini mkataba wa miaka miwili kwa mujibu wa taarifa tuliyonayo.
Alpha ataanza kuonekana kwenye mazoezi ya kikosi cha Yanga siku yoyote kuanzia kesho, Jumatatu.
Aidha kwa upande wa Papi Kabamba Tshishimbi Yanga inatarajiwa kumalizana na klabu ya Mbabane Swallows ndani ya masaa 48.
Yanga tayari imeshamalizana na kiungo huyo raia wa Congo lakini bado ana miezi minne haijamalizika katika mkataba wake na Mbabane.
Jumla ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga ni saba ambao ni Pius Buswita(Mbao), Rostand Youthe Jehu (African Lyon), Ramadhan Kabwili(Azam), Abdallah Shaibu (Taifa Jang'ombe), Ibrahim Ajib (Simba), Raphael Daudi(Mbeya City) na Burhan Akilimali(Huru).
Swala la Gadiel Michael linafanana na Tshishimbi, nae mkataba wake na Azam FC unamalizika mwezi wa 12.
Yanga inatarajiwa kumalizana na Azam FC kabla ya Jumamosi ijayo, siku ya kufungwa dirisha la usajili.

ADVERTISE HERE