Mwananchi tayari umechangia tofali la Ubingwa?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2025
Mwananchi tayari umechangia tofali la Ubingwa?

Katika safari ya mafanikio ambayo Klabu ya Yanga imekuwa nayo kwa misimu minne mfululizo, sasa ni wakati wa mashabiki na wanachama kujitoa kwa vitendo kuhakikisha historia inaendelea kuandikwa. Kupitia kampeni ya Tofali la Ubingwa, kila Mwananchi ana nafasi ya kuwa sehemu ya safari ya kuijenga Yanga imara zaidi kuelekea msimu wa 2025/26.

Tofali la Ubingwa si tofali la kawaida. Ni mchango wa kiuchumi wenye lengo la kuhakikisha Yanga ina msuli mkubwa sokoni katika dirisha hili la usajili. Kila shabiki anayefurahia makombe manne mfululizo na heshima kubwa ndani na nje ya nchi, sasa ana jukumu la kuhakikisha mafanikio haya yanaendelea, kwa kununua tofali lake la ubingwa.

Lengo ni kukusanya tofali milioni 1. Hii itaiwezesha Yanga kusajili wachezaji wa kiwango cha juu, kuimarisha kikosi na kutawala tena, si tu ndani ya Tanzania, bali pia kwenye anga za Afrika kupitia michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Kwa kiasi cha Tsh 24,000/- tu, unaweza kuwa Mwanachama hai wa Yanga SC. Ukiwa mwanachama:

  • Sauti yako itasikika.

  • Utakuwa sehemu ya maamuzi ya klabu.

  • Utachangia maendeleo ya timu unayoipenda.

Kama bado hujajisajili, huu ndio wakati wa kujiunga rasmi. Hii ni nafasi ya kugeuza mapenzi yako kwa klabu kuwa msaada halisi wa maendeleo.

Hatua Rahisi za Kushiriki:

  1. Nunua tofali lako la ubingwa – mchango wako utaongeza nguvu kwenye kampeni hii.

  2. Wasiliana na uongozi, ili ukamilishe mchakato wa kupata kadi yako ya uanachama.

Wananchi, tusibaki kuwa watazamaji. Mafanikio ya kesho yanategemea mchango wako leo. Changia tofali la ubingwa – Tuijenge Yanga imara zaidi!;

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’