Yanga kuikabili Mwadui FC Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2018
Yanga kuikabili Mwadui FC Jumamosi
Baada ya Bodi ya ligi kuu kufanya mabadiliko ya ratiba, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kusafiri kwenda mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom hatua ya lala salama.

Awali Yanga ilitarajiwa kucheza na Mbao FC siku hiyo ya Jumamosi May 19 kwenye uwanja wa Taifa lakini TFF ikaurudisha nyuma mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa siku hiyo ambapo utatumika kuwakabidhi taji mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom, Simba.

Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.

Ratiba ya awali inaonyesha Yanga ilipaswa kucheza na Mwadui FC Jumanne ijayo May 22.

Baada ya mchezo huo Yanga itamaliza michezo yake mitatu iliyobaki dhidi ya Ruvu Shooting, Mbao FC na Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.

Yanga inahitaji kushinda michezo hii ili kuondokana na jinamizi la kucheza michezo mingi bila ya kushinda.

Pazia la ligi kuu litafungwa May 28 ambapo Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kuikabili Azam FC.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’