Kocha Mpya ana ripoti tatu za kuanzia kazi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2025
Kocha Mpya ana ripoti tatu za kuanzia kazi - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa klabu hiyo ina bahati msimu huu baada ya kupokea ripoti tatu za tathmini ya kikosi kutoka kwa makocha waliowahi kuifundisha timu hiyo, kuelekea maandalizi ya msimu wa 2025/26.

Makocha waliowasilisha ripoti hizo ni Miguel Gamondi, Sead Ramovic na Miloud Hamdi. Kamwe amesema baada ya kupokea ripoti hizo, hatua ya kwanza iliyochukuliwa na uongozi wa klabu ilikuwa ni kutafuta kocha mpya kwa haraka, ambaye atalingana na falsafa ya Yanga.

Ameleza kuwa tayari kocha mpya amepatikana na amekabidhiwa ripoti zote tatu kwa ajili ya kuzifanyia tathmini, akilenga kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo, Kamwe amesema klabu haitamtambulisha kocha huyo kwa sasa, ili kuepusha presha isiyo ya lazima katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Kamwe amebainisha kuwa kocha huyo tayari yuko nchini akishirikiana na uongozi katika maboresho ya kikosi

Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki kushiriki kikamilifu kwenye kampeni ya TOFALI LA UBINGWA yenye lengo la kukusanya fedha ambazo zinaweza kutumika katika kusajili wachezaji ww daraja la juu kwa kuzingatia mapendekezo ya kocha mpya

Kampeni hiyo imezinduliwa mapema leo jijini Dar es salaam ambapo leo ni angalau Wanachama MILIONI 1 kulipaa Tsh 24,000

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’