Yanga kushusha kocha kijana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2025
Yanga kushusha kocha kijana

Wakati akizungumza na wanahabari jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alitoa 'code' ya kocha ambaye Yanga wamemuajiri kukiongoza kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria katika msimu ujao

Kamwe alidokeza kuwa kocha huyo ni kijana na mwenye kiu ya mafanikio. Ni kocha ambaye anaendana na mahitaji ya Yanga yenye malengo ya kulisaka taji la Afrika

Kamwe alisema kocha huyo atatambulishwa mwishoni mwa mwezi huu kabla ya timu kuelekea kwenye maandalizi ya msimu mpya

Baada ya kauli ya Kamwe, tetesi zinamuhusisha Romain Folz mwenye umri wa miaka 35) mzaliwa wa Bordeaux huko Ufaransa

Licha ya umri wake mdogo, Romain ni kocha mwenye uzoefu mkubwa katika michuano ya Kimataifa akifanya kazi katika klabu mbalimbali kama kocha mkuu, kocha msaidizi au Mkurugenzi wa ufundi

Mwaka 2024 Folz alihudumu katika klabu ya Mamelodi Sundowns kama Kocha Msaidizi kabla ya kutimkia Algeria kuwa Mkurugenzi wa Michezo klabu ya Olympique Akbou

Folz pia amewahi kuzitumikia ya Guinea Horoya AC (Kocha Mkuu), Amazulu ya Afrika Kusini (Kocha Mkuu), Township Rollers ya Botswana (Kocha Mkuu), Pyramids ya Misri (Kocha Msaidizi) na timu ya Taifa ya Uganda (Kocha Msaidizi)

Folz ana leseni ya juu ya ukocha inayotolewa na UEFA (UEFA Pro Licence) na pia ana Pro Licence ya CONMEBOL

Ukiangalia umri wake na CV yake iliyoshiba, Folz ni kocha aliyewekeza katika kufundisha mpira wa miguu akihitimu mafunzo yake ya ukocha katika umri mdogo

Ni kocha mwingine kijana ambaye anaweza kupata nafasi ya kuinoa Yanga baada ya Cedric Kaze na Sead Ramovic ambao wote wakati wanatua Yanga hakuna aliyewafahamu

Kaze kwa sasa yuko na Nasreddine Nabi katika timu ya Kaizer Chiefs wakati muda mfupi wa kuitumikia Yanga ulitosha kumpa ulaji Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’