Kiungo Clatous Chama raia wa Zambia huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya mazungumzo ya kumuongezea mkataba kutofikia mwafaka, imefahamika
Chama aliyejiunga na Yanga msimu uliopita akisaini mkataba wa mwaka mmoja, yuko huru baada ya mkataba wake kufikia tamati
Yanga ilifungua majadiliano kwa ajili ya kumuongeza mkataba lakini mwafaka haukufikiwa katika upande wa maslahi
Katika msimu wake mmoja na Yanga, Chama alipachika mabao 6 kwenye ligi huku akitoa pasi tatu za mabao
Haikuwa rahisi kwake kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo
Stephane Aziz Ki alikuwa chaguo la kwanza mbele yake na hata Mburkinabe huyo alipotimkia Wydad, Duke Abuya akachukua nafasi na Chama kuendelea kutumika kama mchezaji mbadala katika mechi za mwishoni mwa msimu
Katika dirisha hili Yanga imeongeza zaidi ushindani katika eneo la kiungo ikimsajili fundi Mohammed Doumbia huku pia ikitarajiwa kumuongeza mkataba Duke Abuya wakati Khalid Aucho akiwa amepewa mkataba wa mwaka mmoja