Ni rasmi klabu ya Wydad Athletic imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki baada ya kutimiza masharti ya mkataba baina yake na Yanga, imefahamika
Awali Aziz Ki alijiunga na Wydad kwa mkataba wa muda mfupi ambapo klabu hiyo ilipaswa kukamilisha mchakato wa usajili kabla ya Julai 10
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imethibitisha kuwa Wydad tayari wamewasiliana na Yanga kwa ajili ya kukamilisha usajili huo
Yanga sasa inatarajiwa kuvuna takribani Bil 1.7 katika usajili wa MVP na mfungaji bora huyo wa ligi kuu ya NBC msimu wa 2023/24
ADVERTISE HERE