Yanga ina miezi miwili kabla ya kuivaa Gor Mahia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 May 2018
Yanga ina miezi miwili kabla ya kuivaa Gor Mahia
Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila ya kufungana na Rayon Sports leo, Julai 18 2018 Yanga itasafiri nchini Kenya kuivaa Gor Mahia kwenye mchezo wa tatu wa kundi D.

Jana Gor Mahia ilikuwa nyumbani ikalazimishwa suluhu ya bila kufungana na USM Alger ambayo sasa inaongoza kundi D ikiwa na alama nne.

Kimahesabu Yanga bado inaweza kutinga robo fainali ya michuano hiyo kama zilivyo timu zote za kundi D.

Iwapo Yanga itaweza kutumia vizuri muda wa miezi miwili kujiandaa vyema inaweza kwenda kupata matokeo nchini Kenya kabla ya timu hizo kurudiana jijini Dar es salaam baada ya siku 10.

NINI KIFANYIKE?

Kwa hali ilivyo Yanga inalazimika kujaza nafasi zake tatu haraka iwezekanavyo ili wachezaji hao watakao-ongezwa wawe na muda wa kutosha kuzoeana na wenzao.

Ikiwezekana ili wachezaji hao waweze kutumika kwenye mchezo ujao dhidi ya Gor Mahia

Yanga inahitaji kumalizana haraka na Lipuli kumpata Salamba au apatikane mshambuliaji mwingine mwenye uwezo wa kuzifumania nyavu na pia inahitaji kuimarisha safu yake ya kiungo.

Kiungo ndio 'engine' ya timu yoyote. Kwa sasa Yanga inakosa kiungo 'mwenye macho', mchezeshaji mwenye uwezo wa kupiga pasi za mwisho.

Yanga haiwezi kuwategemea Thabani Kamusoko ambaye ndiyo kwanza anaanza kurejea kwenye kiwango chake na Papi Tshishimbi anayesumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara yanayotokana na 'kutumika' kwa muda mrefu.

Wakipatikana viungo wawili mahiri na Mshambuliaji mmoja wanatosha kuifanya Yanga iwe tofauti.

Kwenye mchezo wa leo tumeishuhudia Yanga ambayo inaweza kushambulia kwa kasi kilichokosekana ni mipira ya mwisho ya kuweza kuzalisha mabao.

Bado Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hii kwani 'on paper' haitofautiani sana na wapinzani wake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’