Yanga yafafanua makubaliano na Wydad usajili wa Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2025
Yanga yafafanua makubaliano na Wydad usajili wa Aziz Ki

Klabu ya Yanga imetoa ufafanuzi juu ya makubaliano ya uhamisho wa kiungo mshambaliaji wa timu hiyo Stephane Aziz Ki aliyesajiliwa na Wydad Athletic

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema Yanga iliingia makubaliano ya aina mbili na Wydad katika mchakato wa usajili wa kiungo huyo

Kamwe amefichua kuwa mpaka sasa Aziz Ki bado ni mchezaji wa Yanga ambaye anaitumikia Wydad kwa mkopo wa miezi mitatu na Wydad wana hadi Julai 10 2025 kumsajili moja kwa moja

"Mkataba ambao Stephane Aziz Ki aliusaini au sisi ambaao klabu tuliusaini na Wydad Casablanca wakati tunamuuza, ulikuwa ni mkataba wenye vipengele viwili"

"Cha kwanza ulikuwa ni mkataba ambao una makubaliano ya miezi mitatu, wakiwa wameridhishwa baada ya kiwango chake kwenye kombe la Dunia la klabu, wataurefusha kwenda miaka miwili"

"Kwa hiyo ile miezi mitatu ya kwanza kuna kiasi walikilipa kwa klabu ili tuwape 'release letter' na kumruhusu mchezaji aende akacheze na kwa mujibu wa makubaliano ilikuwa tarehe 10 Julai wawe wamewasiliana na klabu yetu kama watakuwa wanamuhitaji maana yake wamalizie kile kiasi ambacho tulikubaliana kwenye mkataba"

"Lakini kama wakiona wameshindwa, Aziz Ki atarudi nyumbani kwa sababu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Yanga"

"Tulisema tuiache taarifa hiyo kwanza ili kijana aende kucheza kombe la Dunia la klabu na kwa kuwa Wydad walitulipa fedha ya makubaliano ya awali kwa sasa tunasubiri hatma yao ambayo kwa mujibu wa mkataba ni Julai 10"

"Kama wameridhishwa nae wanapaswa kutulipa fedha yetu tuliyokubaliana lakini kama hawakuridhika nae, kijana atarudi nyumbani kuendelea kuwashona watu," alitamba Kamwe

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, ifikapo Julai 11, kama Wydad hawatakuwa wamewasiliana na Yanga, Aziz Ki atarejea kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
32m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’