Klabu ya Yanga, imemshukuru aliyekuwa kocha wake Miloud Hamdi ambaye jana alitambulishwa katika klabu ya Ismaily ya nchini Misri.
Kocha huyo alijiunga na Yanga katikati ya msimu uliomalizika hivi karibuni na kufanikiwa kutwaa mataji matatu nchini yake.
Taji la kwanza lilikuwa Kombe la Muungano, taji la pili ni NBC Premier League na taji la tatu ni CRDB Bank Federation Cup.
Kocha huyo alitua Yanga akitokea Singida BS na alipokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake Sead Ramovic.

KILA LA KHERI HAMDI..!
ADVERTISE HERE