Viongozi Lipuli FC wakutana kumjadili Salamba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2018
Viongozi Lipuli FC wakutana kumjadili Salamba
Uongozi wa Lipuli Fc tayari umekutana kujadili ombi la klabu ya Yanga la kumtaka mshambuliaji wake Adam Salamba ili aongezwe kwenye kikosi cha klabu hiyo kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga imedhamiria kuongeza wachezaji watatu kukiongezea nguvu kikosi chake. Nafasi hizo imezipata baada ya kuwa ilisajili wachezaji 27 mwanzoni mwa michuano hiyo.

Kila timu inayofuzu michuano ya CAF ngazi ya vilabu inaweza kusajili mpaka wachezaji 30 kushiriki michuano hiyo.

Mwenyekiti wa Lipuli FC Ramadhan Mahano amethibitisha juu ya timu yake kulijadili ombi hilo na kueleza kuwa hawatakuwa na pingamizi kumruhusu Salamba kuitumikia Yanga kwenye michuano hiyo ya CAF iwapo mchezaji mwenyewe atakubali na timu hizo zikafikia makubaliano.

Mahamo amesema hawawezi kumzuia Salamba kuitumikia Yanga kwani kufanya hivyo itakuwa kumnyima fursa adimu.

Mohamo ameongeza kuwa hata kama Yanga itataka kumsajili mchezaji huyo moja kwa moja, wao hawana pingamizi kama klabu hiyo itafuata taratibu za usajili wakati utakapofika.

Mbali na Yanga, Salamba amekuwa akiwindwa na klabu ya Azam FC.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’