Wakati kesho Jumapili Yanga ikitarajiwa kushuka uwanja wa New Amaan Complex kuikabili Singida Black Stars katika mchezo wa fainali ya kombe la CRDB, maandalizi ya paredi ya ubingwa tayari yameanza
Gari maalum la paredi kutoka Uganda ambalo limetumika kwa misimu mitatu, tayari liko njiani
Yanga itashuka dimbani hapo kesho kusaka taji la tano msimu huu, manne yakiwa tayari yanasubiri paredi tu
Toyota Cup, Ngao ya Jamii, Muungano Cup na Ligi Kuu haya hayana kipengele na yatatambulishwa mbele ya Wananchi katika paredi ambayo itafanyika jijini Dar es salaam mapema wiki ijayo
Kazi iliyobaki ni kuhakikisha Yanga inabeba taji la CRDB hapo kesho kwa msimu wa nne mfululizo ili kukamilisha malengo ya msimu
ADVERTISE HERE