Hamdi anaendelea kuweka rekodi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2025
Hamdi anaendelea kuweka rekodi Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameendelea kudhihirisha Rais wa Yanga Injinia Hersi Said hakufanya makosa kumfuata Singida BS kikosi chake kikiendelea kugawa dozi

Baada ya kuiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopita, Hamdi leo ameiongoza tena Yanga kuibuka na ushindi mwingine wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa

Tangu atue Yanga baada ya kuondoka ghafla kwa Kocha Sead Ramovic, Hamdi ameiongoza Yanga katika mechi 16 za mashindano ambapo ameshinda 15 na sare moja tu

Katika kipindi chake Hamdi pia ameiongoza Yanga kutwaa taji la Muungano mwezi May mwaka huu

Hamdi amebakisha mechi mbili muhimu ambazo kama atashinda zote, ni wazi atajihakikishia mkataba wa muda mrefu na Wananchi

Ikumbukwe wakati anatua Yanga, Hamdi alisaini mkataba wa muda mfupi ambao utafikia tamati baada ya mchezo wa fainali kombe la CRDB dhidi ya Singida BS utakaopigwa Juni 29

Kazi aliyobakisha kwake ni kuhakikisha Yanga inatetea taji la ligi kuu na CRDB

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
44m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’