Hamdi afurahi dabi kurejea, asema Yanga ipo tayari kumaliza kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
16 Jun 2025
Hamdi afurahi dabi kurejea, asema Yanga ipo tayari kumaliza kazi

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi, amesema kikosi chake kiko tayari kwa hatua ya mwisho ya msimu huu, akifurahia kurejea kwa mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba maarufu kama Kariakoo Dabi baada ya sintofahamu ya ratiba kuisha.

Hamdi amesema hayo kuelekea mchezo wa Jumatano, Juni 18 dhidi ya Tanzania Prisons, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Huo utakuwa ni mchezo wa kwanza kati ya minne ya mwisho kwa Yanga msimu huu, ukiwa ni sehemu ya safari yao ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu na kutwaa kombe la CRDB.

“Tunaziheshimu timu zote, hapo kabla hatukuwa na ratiba ya mechi dhidi ya Simba, lakini sasa mambo yamekuwa wazi. Tupo tayari kwa mchezo huo na tutahitaji kushinda kama tulivyoshinda mechi zingine,” alisema Hamdi.

Yanga bado ina mechi tatu za Ligi Kuu:

  1. Tanzania Prisons – Juni 18, Uwanja wa Sokoine

  2. Dodoma Jiji – Juni 22, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

  3. Simba SC – Juni 25, Uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya ligi, Yanga itamaliza msimu kwa kucheza fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars mnamo Juni 28.

Hamdi alieleza kuwa kurejea kwa mechi ya dabi kumeongeza morali kambini huku akisisitiza ubora wa kikosi chake ambacho kimeweza kuifunga kila timu msimu huu angalau mara moja jambo alilolieleza kama ishara ya kiwango cha juu walicho nacho.

“Unajua Yanga ndiyo timu pekee ambayo imezifunga timu zote msimu huu angalau kwa mchezo mmoja. Unapoona rekodi kama hii, unapata tafsiri sahihi ya ubora wa kikosi chetu. Tunataka kushinda mechi zote zilizosalia,” aliongeza Hamdi kwa kujiamini.

Mashabiki wa Yanga sasa wana kila sababu ya kutazamia msimu wa mafanikio kama kikosi chao kitaendeleza kasi ya ushindi hadi mwisho. Dabi ya Juni 25 si tu fursa ya kulinda heshima, bali inaweza kuwa kilele cha kutawazwa mabingwa kwa mara ya 31.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →